1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAFAH: Mwanachama wa Fatah ameuawa kwa risasi

6 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5l

Mwanachama wa chama cha Fatah cha rais Mahmoud Abbas,ameuawa katika mapambano mapya yaliyozuka kati ya Wapalestina kwenye Ukanda wa Gaza.Mtu mwenye silaha asiejulikana alimpiga risasi Mpalestina huyo baada ya sala ya jioni mjini Rafah.Muda mfupi baadae,mfuasi wa kundi hasimu la Hamas,alijeruhiwa vibaya katika shambulio jingine.Mapigano ya hivi karibuni kati ya Fatah na Hamas yameua zaidi ya Wapalestina 10,huku kinyanganyiro cha madaraka kikiendelea kati ya makundi hayo mawili.