1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wahama makazi kukimbia mapigano Kongo

Zainab Aziz
14 Februari 2024

Raia wanahama kwa wingi na kuelekea katika mji wa Goma nchini Kongo wakati ambapo mapigano yanaendelea katika maeneo jirani ya mji wa Sake, Malehe na Kashaki na kutoka kwenye vijiji mbalimbali vya eneo la Masisi.

https://p.dw.com/p/4cP4f
DR Kongo | Wakaazi wakiukimbia mji kutokana na mapigano
Wakongomani wakiwa na mizigo wakikimbia mji kutokana na mapiganoPicha: Benjamin Kassembe/DW

Mji wa Sake, ndio uliokuwa na idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wa ndani katika eneo la Kivu Kaskazini. Kwa sasa mji wa Goma una zaidi ya wakimbizi milioni moja wa ndani.

Msimamizi wa misaada katika mji wa Goma Marc Sere de Rivieres, amesema hali ni ngumu mno na baadhi ya wafadhili wamelazimika kusimamisha shughuli zao.

soma pia:Kongo: Mji wa Sake haujadhibitiwa na waasi

Ametahadharisha juu kutokea mgogoro wa kibinadamu ambao amesema unaweza kusababisha maafa makubwa na ameitaka jumuiya ya kimataifa ichukue hatua za haraka ili kupeusha maafa zaidi.