1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Chavez tena amegonga vichwa vya habari

13 Mei 2008

Rais wa Venezuela Hugo Chavez hupenda kuzichochea Marekani na Umoja wa Ulaya;kuziponda nchi za Magharibi na kuugawa ulimwengu kati ya wabaya na wazuri.

https://p.dw.com/p/DzH2
Bundeskanzlerin Angela Merkel eroeffnet am Mittwoch, 7. Mai 2008 die woechentliche Kabinettssitzung im Bundeskanzleramt in Berlin. (AP Photo/Markus Schreiber) *** In this photo released by Miraflores Press Office, Venezuela's President Hugo Chavez speaks on his weekly radio and television show "Hello President" in Maracaibo, Venezuela, Sunday, May 11, 2008. Chavez said that the documents Colombia unveiled as proof that he sought to help arm and finance Colombian rebels are fake. (AP Photo/Miraflores Press Office)
Picha ya kushoto yamuonyesha Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.Kulia ni Rais wa Venezuela Hugo ChavezPicha: AP

Ni jambo la kawaida kwa matamshi ya Rais Chavez kugonga vichwa vya habari muda mfupi tu kabla ya kufanywa mikutano mikubwa ya kimataifa.

Safari hii pia kabla ya kufanywa mkutano wa kilele wa nchi za Umoja wa Ulaya na Amerika Kusini,Rais wa Venezuela Hugo Chavez amevuma upya baada ya kiongozi huyo kumlinganisha Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Adolf Hitler.Ingawa rais wa Venezuela anaefuata siasa za mrengo wa shoto anajulikana kwa ulimi wake mkali,safari hii amevuka mpaka,kwani kumlinganisha Merkel na Hitler si utovu wa nidhamu tu bali ni upumbavu mtupu.Na jinsi Kansela Angela Merkel alivyopuuza matamshi ya Chavez kumedhihirisha upumbavu wa linganisho hilo.

Kilichomhamakisha Rais Hugo Chavez hadi kufanya linganisho hilo,ni mahojiano yaliyofanywa na Kansela Merkel pamoja na shirika la habari la Ujerumani-DPA kabla ya kuanza ziara yake ya mwanzo kabisa katika nchi za Amerika Kusini tangu kushika madaraka,zaidi ya miaka miwili iliyopita.Katika mahojiano hayo Merkel alisema,Chavez hazungumzi kwa niaba ya nchi za Amerika Kusini,kwani kila nchi katika kanda hiyo ina sauti yake na kuambatana na maslahi yake.

Lakini Merkel alitamka ukweli wa mambo alivyoeleza matatizo ya kimsingi katika uhusiano wa nchi za Umoja wa Ulaya na Amerika Kusini.Kwani majadiliano yanayohusika na biashara huru yamekwama kwa sababu kila nchi inatoa umuhimu zaidi kwa maslahi yake badala ya kuwa na malengo ya pamoja kwa kanda nzima.Sasa nchi za Ulaya zimeanza kuzipa kisogo nchi za Amerika Kusini.Kwa mfano tangu muda mrefu uchumi wa Ujerumani unajishughulisha zaidi na masoko ya Bara la Asia.Hata Bara la Afrika kijiografia,lipo karibu zaidi na Ulaya:matatizo ya kijamii ya Bara la Afrika yamefika mlangoni Ulaya.Kwa hivyo ni dhahiri kuwa nchi za Ulaya zikizingatia maslahi yake zinajishughulisha zaidi kupiga vita umasikini katika nchi zilizo kusini mwa Sahara.

Kwa upande mwingine,katika Amerika Kusini kuna ukosefu mkubwa sana wa haki za kijamii kuliko mahala pengine popote pale duniani.Iwapo,au kwa umbali gani,Rais Hugo Chavez ataweza kujitokeza kama msemaji wa nchi za Amerika Kusini,hutegemea kwa umbali gani atafanikiwa kupata ufumbuzi wa masuala ya kijamii katika kanda hiyo.

Wakati huo huo ikiwa Umoja wa Ulaya hautotia maanani msimamo wa nchi kama vile Argentine,Bolivia na Ecuador zinazopinga soko huru na mashirika ya fedha ya kimataifa,basi majadiliano kati ya nchi za Ulaya na Amerika Kusini hayatokuwa na matokeo yo yote.