1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Kagame aelekea kushinda kwa kishindo uchaguzi wa rais Rwanda

Josephat Nyiro Charo10 Agosti 2010

Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi rais Kagame amejishindia asilimia 92.9 ya kura kutoka wilaya 11

https://p.dw.com/p/Ogh4
Wafuasi wa rais Paul Kagame na chama chake cha RPF wakishangiliaPicha: picture-alliance/dpa

Matokeo ya awali katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Rwanda hapo jana yameonyesha kuwa Rais wa sasa Paul Kagame ameshinda kwa kishindo, akipata asilimia 92.9 ya kura zote. Mpinzani wake wa karibu kutoka chama cha Social Democrats Jean Damascene Ntawukuriryayo amejinyakulia asilimia 4.9, na chama chake kimetangaza kuwa kitakubali matokeo. Matokeo hayo ya awali yamepatikana baada ya kuhesabu kura kutoka wilaya 11 kati ya 30 za nchi hiyo.

Kwa maelezo zaidi huyu hapa mwandishi wetu mjini Kigali, Daniel Gakuba.

Mwandishi: Daniel Gakuba

Mhariri:Josephat Charo