1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Obama aongoza Kumbukumbu ya mashambulio ya September 11 nchini Marekani.

Jane Nyingi/ AFPE..Picha AFP11 Septemba 2009

Wamarekani leo wanakumbuka miaka minane tangu magaidi wa kundi la Al Qaeda walipofanya mashambulio ya kigaidi.

https://p.dw.com/p/JdHB
Kituo cha World Trade Centre kilichoshambuliwa na magaidi September 11 miaka minane iliyopitaPicha: AP

Magaidi hao wakitumia ndege walikishambulia kituo cha World Trade Centre mjini Newyork,pamoja na makao makuu ya wizara ya ulinzi , Pentagon mjini Washington. ambapo karibu watu alfu 3 waliuawa.Ibada za kuwakumbuka waliopoteza maisha yao zimepangwa kufanyika leo kote nchini humo. Kutoka Washington nimezungumza na mhadhiri wa Chuo kikuu Dr Nicholas Boaz ambaye kwanza anaelezea jinsi siku hiyo ya msiba mkubwa inavyokumbukwa hii leo.