1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Putin akutana na waziri mkuu wa Poland Tusk

9 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D4td

Moscow:

Rais Vladimir Putin wa Urusi na waziri mkuu wa Poland Donald Tusk wameelezea azma ya kurekebisha uhusiano uliopooza kwa muda mrefu kati ya nchi zao.

Baada ya mazungumzo yake pamoja na rais Vladimir Putin mjini Moscow,waziri mkuu Donald Tusk amesema wamedhamiria kushirikiana ili kusaka ufumbuzi wa masuala kadhaa tete yaliyopo.Waziri mkuu wa Poland Donald Tusk amesisitiza hata hivyo nchi yake inapinga moja kwa moja mipango ya Urusi na Ujerumani kujenga mabomba ya kusafirishia gesi kupitia bahari ya mashariki.