1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Talabani wa Iraq ataka uwekezaji wa Uturuki

8 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DL9O

ANKARA

Rais Jalal Talabani wa Iraq katika ziara yake ya kwanza nchini Uturuki akiwa kiongozi wa taifa amewataka wafanya biashara wa Uturuki kuwekeza kwa wingi nchini Iraq.

Talabani amesema lengo la Iraq ni kuwa na ushirikiano thabiti na utakodumu kwa muda mrefu na Uturuki katika ngazi zote.Ziara yake pia imekusudia kupunguza hali ya mvutano kufuatia mashambulizi ya Uturuki ya kuvuka mpaka wa Iraq kuwashambulia waasi wa Kikurdi wa kundi la PKK kaskazini mwa Iraq.

Hapo jana Talabani na Rais wa Uturuki Abdullah Gul wameapa kuendelea kuchukuwa hatua dhidi ya kundi hilo la PKK.