1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa China Huo Jintao atahadharisha mafisadi

Tuma Provian Dandi15 Oktoba 2007

Rais wa China Bwana Hu Jintao ametoa tahadhari kwa viongozi wa serikali kuhusu ufisadi. Hayo kamo katika hotuba aliyoitoa wakati wa Wiki ya Baraza Kuu la nchi hiyo linalofanyika kila baada ya miaka mitano.

https://p.dw.com/p/C7hn
Rais wa China Hu Jintao akihutubia
Rais wa China Hu Jintao akihutubiaPicha: AP

Akisoma hotuba yake kwa umma wa raia wa China wapatao elfu 2 na 200, Rais wa nchi hiyo Bwana Hu Jintao amesisitiza kuendelea kukabiliana na sera zilizopo ili kuwezesha kuwa na uchumi imara zaidi na kushughulikia matatizo ya wananchi.

Akiwa mfuasi wa itikadi za Kikomonist, Rais Jintao ameahidi kuendelea kukabiliana na vitendo vya rushwa na ufisadi katika serikali yake ikiwemo kuweka mikakati imara itakayokuwa mwongozo wa kuleta mageuzi kamili katika nyanja zote.

Aidha, Rais Hu Jintao wa China amesema Baraza kuu la nchi hiyo litakuwa na wajibu wa kuwasilisha ripoti zote kwa kamati kuu na kwamba Baraza kuu litalazimika kukubali udhaifu wowote utakaobainika baada ya mapandekezo ya Kamati kuu.

Katika kukomesha vitendo vya rushwa na ufisadi, tayari kiongozi mmoja wa chama cha Shanghai, Bwana Chen Liangyu, amepoteza wadhifa wake ambapo sasa anakabiliwa na kesi ya rushwa.

Aidha, Baraza kuu la China limeshamwajibisha mwanasiasa mwingine wa chama hicho Bwana Chen Xitong aliyefungwa kwa miaka 16 kutokana na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Raia Hu Jintao ameahidi kuwa mkali katika uchaguzi wa Kamati Kuu utakaofanyika wiki ijayo kwa kukabiliana na rushwa, na kwamba ataufanya kuwa wa kidemokraisa.

Katika hotuba yake Rais Jintao amesema viongozi wengi katika chama chake wanakabiriwa na tuhuma mbalimbali hasa za rushwa na kutowajibika vema ikiwemo kujilimbikizia mali nyingi, huku raia wakikosa mahitaji yao ya msingi.

Uchunguzi unaonesha kwamba china ina kiasi kikubwa cha watu wasiokuwa na ajira, makazi salama, elimu nzuri pamoja na huduma ya afya.

Akieleza kuhusu mafanikio cha China katika kilele cha Baraza kuu litakalochukua juma zima, Rais Hu Jintao amesema hawana budi kufanya kazi kwa bidii ili kuzidi kuyafanya maisha ya wananchi wao kuwa mazuri zaidi na kwamba huu siyo wakati wa kubweteka kutoka na hali mzuri ya uchumi uliopo kwa sasa.

Maadhimisho ya wiki ya Baraza kuu la China pia yamehudhuriwa na Rais mstaafu Jiang Zemin aliyekuwa ameketi pembeni ya Rais wa sasa Hu Jintao.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini humo wanasema huenda Rais Hu Jintao anatumia mwanya huu kumwandaa rais atayechukua nafasi yake baada ya kumaliza kipindi chake hapo mwaka 2012.

Maadhimisho ya Baraza kuu la China linalofanyika kila baada ya miaka mitano yameanza kwa wanajeshi wa nchi hiyo kuimba wimbo wa taifa, pamoja na kukumbuka mchango wa waasisi wa chama cha Kikomonist kilichoifikisha China hapo ilipo katika masuala ya uchumi.

Rais Hu hakuficha hali halisi ya chama chake cha Kikomonist ikiwemo matatizo yanayokikumba, amesema pamoja na mapungufu ya kawaida, atatumia kila uwezo wake kuunda sera mpya zitazosaidia maendeleo zaidi.

Kiongozi huyo wa kikomonist amesisitiza kauli yake kuwa bado Beijing ina nguvu juu ya Taiwan, na kwamba hakuna mtu yeyote, kikundi wala nchi itakaiondoka kisiwa cha Taiwan katika ramani ya China.