1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa DFB ajiuzulu

Admin.WagnerD10 Novemba 2015

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo(10.11.2015) wameandika juu ya kujiuzulu kwa rais wa shirikisho la soka la Ujerumani DFB, Wolfgang Niersbach, mvutano uliojitokeza katika serikali ya mseto kuhusu sera za wakimbizi.

https://p.dw.com/p/1H3Gl
Deutschland DFB Präsident Wolfgang Niersbach Rücktritt
Rais wa zamani wa DFB Wolfgang Niersbach akitangaza kujiuzuluPicha: Reuters/R. Orlowski

Na pia wamejishughulisha na maandamano ya kundi linalopinga wahamiaji PEGIDA mjini Dresden jana(09.11.2015).

Gazeti la Stuttgart Nachrichten, likiandika kuhusu kujiuzulu kwa rais wa shirikisho la kandanda nchini Ujerumani , gazeti linaandika.

"Kwa muda mrefu ilionekana kwamba Wolfgang Niersbach anataka kupambana hadi katika dakika za nyongeza. Lakini pia inaonekana rais huyo wa DFB alionekana kuchukua mtazamo wa kupambana na wakosoaji wake, lakini hatimaye amekubali kushindwa. Kujiuzulu kwake ni firimbi ya ghafla ya kumaliza mchezo , ambao kila wakati kulikuwa na taarifa zinazomlazimisha kurejea katika nafasi ya kujihami zaidi kuliko kushambulia."

Shutuma kuhusu rushwa ili kupatiwa Ujerumani fursa ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia zimekuwa kubwa, na maswali magumu yaliyomuandama Niersbach hakuweza kuyajibu , linaandika gazeti la Braunschweiger Zeitung.

"Mbinyo ulikuwa unaongezeka zaidi na zaidi, kiasi kwamba kiongozi huyo ama hakutambua kabisa ama kwa kiasi fulani hakuna na habari. Kiongozi huyo wa DFB aliyekuwa akiyumba yumba katika matamshi yake, hakutambua , ni wapi litatokea shambulio jingine linaloweza kumbwaga chini. Hilo halikuwa mbali , hususan jana zilipojitokeza shutuma nyingine mpya. Kabla ya kuoneshwa kadi nyekundu, aliamua binafsi kujitoa. Hakuwa na fursa nyingine."

Suala lingine lililoandikwa katika magazeti ya Ujerumani ni kuhusu sera za wakimbizi. Sera kwa ajili ya wakimbizi za muungano mkuu katika serikali mjini Berlin zinakumbusha filamu inayoitwa "Kila siku namsalimu panyabuku". Mhariri wa gazeti la Rheinishe Post anaandika.

"Katika filamu hiyo kuna hadithi ambayo mtu mmoja anasimulia , kile ambacho kila siku anakumbana nacho. Mhariri anandika , Kila inapotolewa idadi ya wakimbizi wanaoingia nchini Ujerumani, katika serikali ya mseto linajirudia suala maalum, ambao ni suali la familia za wakimbizi. Kiongozi mwandamizi katika serikali hiyo ya mseto ametoa wazo la kushangaza. Chama cha SPD kilichomo katika muungano huo wa serikali kimefadhaishwa nalo. Upinzani unasema ni kinyume na ubinadamu. Serikali ya mseto imo katika mvutano."

Kiwango cha mzozo huo wa wakimbizi hatimaye , kinataka pachukuliwe hatua za kuweka ukomo.

Kutokana na kuelemewa maafisa kwa hivi sasa ndugu wa wakimbizi hawatachukuliwa. Lakini kila inapokuwa mkimbizi anabakia kwa muda mrefu zaidi ndipo uwezekano wa kutambuliwa unakuwa mkubwa zaidi na ndivyo suala hili litakavyozidi kupata nguvu.

Nae mhariri wa gazeti la Berliner Zeitung anazungumzia mjadala kuhusu wakimbizi kuwaleta ndugu zao nchini Ujerumani.

Pegida marschiert in Dresden
wafuasi wa PEGIDA wakiandamana mjini DresdenPicha: Picture-alliance/dpa/A. Burgi

"Ni sawa kuwachukua wakimbizi wa Syria wanaokimbia vita nchini kwao, ni jambo sahihi kabisa na la kiutu. Ni suala linalowahusu wale tu ambao wanahitaji msaada. Ni hali ya kusikitisha ya watu wasio kuwa na uwezo dhidi ya wanasiasa, ambao wanatakiwa kuendeleza misingi yao ya maadili ya kikristo."

Kuhusu suala la maandamano ya kundi linalopinga wahamiaji la PEGIDA , mhariri wa gazeti la Neue Osnabrücker anauliza:

"Hakuna fadhaa katika siku ya fadhaa", Mjini Dresden kwa bahati mbaya hakuna wazo hilo la kidini. Kwa mara nyingine tena wamekusanyika maelfu ya wafuasi wa kundi hilo lenye utata la vuguvugu la PEGIDA. Na kumekuwa na matamshi ya kupinga wahamiaji na Uislamu. Na hususan katika siku ya kumbukumbu ya tarehe 9 Novemba . Siku hiyo wakifanya uharibifu wa kuchoma moto majumba na mali, unyanyasaji, kuwakamata watu na kuwauwa, wafuasia wa Wanazi na watu wengine wengi waliongoza uharibifu huo usiku wa Novemba 9 kuamkia Novemba 10 mwaka 1938 wakifanya uhalifu huo dhidi ya Wayahudi. Kwa mamilioni ilikuwa na maana ya mwanzo wa mwisho. Na katika siku kama hiyo kulikuwa na matendo kinyume na ubinadamu na ilikuwa ni aibu tupu."

Mwandishi: Sekione Kitojo / inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman