1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa FIFA A.Kusini

18 Septemba 2008

Sepp Blatter amaliza ziara yake ya siku 4 na amefurahishwa na jinsi maandalio yanavyosonga mbele.

https://p.dw.com/p/FKsa
FIFA president Joseph S. BlatterPicha: picture-alliance/ dpa

Rais wa FIFA -Shirikisho la dimba ulimwenguni -Sepp Blatter, akimaliza ziara yake ya Afrika kusini ya kukagua viwanja vitakavyochezewa kombe lijalo la dunia 2010,aonesha ameridhika na aliojionea na ahadi alizopewa kuwa kila kitu kitakuwa tayari kwa kombe hilo.

Kwa wafanyikazi wanaojenga viwanja na zana nyengine ,Blatter amewaahidi tiketi za bure kuangalia dimba ikiwa kama shukurani kwa kazi wanaoifanya.

Nje ya maandalio ya kombe la dunia,kinyanganyiro kitapamba moto kesho jumamosi na jumapili kuania nafasi za nusu-finali ya kombe la klabu bingwa barani Afrika-champions League.

►◄

"Nimefurahishwa sana." Rais wa FIFA alisema hayo baada ya kuzuru Ellis Park Stadium,uwanja uliopo jijini Johannesberg-mmoja kati ya viwanja 2 katika jiji hilo vinavyotengezwa upya kwa ajili ya kombe la dunia.

Akieelezea furaha yake ya kuwa tena Afrika kusini,rais wa FIFA alisema anapendelea sana midundo ya Afrika kusini tofauti na ile ya nyumbani Uswisi inayokaliwa na wanaozungumza kijerumani.

Wakati wa ziara yake ya siku 4,Blatter alikutana na na mzee Mandela aliekuwa ufunguo wa kushinda Afrika kusini kuandaa kombe hilo lijalo la dunia na la kwanza kabisa kuandaliwa barani Afrika.Halkadhalika, alionana na rais Thabo Mbeki.

Rais wa FIFA alizima hofu za kuzuka uhalifu mkubwa nchini Afrika kusini ambazo zingewafanya mashabiki wengi wa kombe la dunia kutokwenda kuangalia dimba.Inakisiwa hadi watu 50 wanauwawa kila siku.

Ama kuhusu kutocheza uzuri wakati huu kwa Bafana Bafana-timu ya taifa ya Afrika kusini,Sepp Blatter anatazamia wenyeji watateremsha timu kali litakapoanza kombe la dunia .Blatter alitangaza kwamba wafanyikazi 20.000 wanaohusika na ujenzi wa viwanja 10 vya kombe la dunia katika miji 9 mbali mbali kila mmmoja atapewa tiketi 2 bure kuangalia mechi .

Nje ya kombe la dunia, kinyanganyiro cha kuania tiketi za kucheza nusu-finali ya kombe la klabu bikngwa barani Afrika , kinarudi uwanjani mwishoni mwa wiki hii.Kwani jumla ya klabu 7 zinatapia nafasi hizo zikitumai kujiunga na Al ahly ya Misri.

Kwa msangao wa wengi Dynamo ya Zimbabwe inajikuta katika hali bora kabisa kujiunga na Al Ahly kutoka kundi lake A kwani ushindi dhidi ya zamalek jumapili hii utawafikisha mbali.Wakitoka sare mjini Harare utawsafungulia mlango ASEC Mimosa wa Ivory Coast kuwapiku mahasimu wote wawili mradi tu wafanye maajabu ya kuwashinda mabingwa mara kadhaa Al Ahly.

Zamalek kwa upande wake watasonga mbele na mwishoe, kunyakua kitita cha dala milioni 3.5 cha klabu bingwa ikiwa wataitimua nje Dyanamo.

Dynamo ndio iliowapiga kumbo mabingwa Etoile du sahel ya Tunisia.

Al Hilal ya Sudan ina miadi na TP mazembe hii leo ijumnaa katika kundi B -mpambano utakaofuatiwa na ule kati ya Contonsport garoua ya Kamerun ikiikaribisha Enyimba ya Nigeria nyumbani.

Enyimba pamoja na TP Mazembe na Al Ahly ndio timu pekee zilizotetea mataji yao tangu kinyanźganyiro hiki kuanzishwa miaka 43 iliopita.Wana jumla ya pointi 9 wakati Mazembe na Al hilal 5 kila moja.sare nchini Kamerun itawahakikishia Enyimba nafasi ya nusu-finali.

Nusu finali zimepangwa Oktoba 3-5 na duru ya pili oktoba 17 hadi 19.

Washindi watacheza finali ya duru 2 huku mshindi akitoroka na kitita cha dala milioni 1 na mualiko wa kucheza katika kombe la dunia la klabu bingwa nchini Japan.