1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Korea Kusini akabiliwa na mtihani mgumu

Mohammed Khelef
10 Aprili 2024

Korea Kusini inafanya uchaguzi muhimu wa bunge, unaochukuliwa na wengi kuwa kama kura ya maoni kwa uongozi wa Rais Yoon Suk Yeol. Utafiti wa maoni ya wapigakura unaonesha vyama vya upinzani vitaendelea kulihodhi bunge.

https://p.dw.com/p/4ebDF
Korea Kusini
Rais wa Korea Kusini Rais Yoon Suk YeolPicha: KIM MIN-HEE/Reuters

Tangu alipoingia madarakani mwaka 2022, muendesha mashitaka huyo wa zamani amekuwa na uungwaji mkono wa kiwango wa chini, huku wapinzani wake wa kiliberali wenye wingi wa viti bungeni wakikwamisha ajenda zake za mageuzi.

Endapo chama chake cha kihafidhina kitashindwa kwenye uchaguzi wa, Yoon ataendelea kuwa rais asiye na nguvu ya kubadili chochote hata kama ataendelea kusalia madarakani.

Hata hivyo, waangalizi wa uchaguzi wanasema bado ingali mapema kutabiri matokeo ya mwisho, kutokana na tabia ya wapigakura wa Korea kufanya maamuzi dakika za mwisho. Bunge la korea Kusini lina viti 300.