1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Mali ahimiza hatua za haraka

20 Oktoba 2012

Rais wa mali Dioncounda Traore amesema kuwa, sekunde moja haipaswi kupotezwa katika kulikamata eneo la kaskazini mwa nchi hiyo kutoka kwa waasi wa Kiislamu ,wakati mkutano na viongozi wa mataifa ya Afrika na Ulaya.

https://p.dw.com/p/16Tcl
African Union Chief Nkosazana Dlamini-Zuma (front L) and Mali's President Dioncounda Traore attend a high level international meeting in Bamako, October 19, 2012. Regional leaders joined international organisations in Bamako on Friday trying to narrow their differences over whether al Qaeda-linked Islamists in the north of Mali should be dislodged via military intervention or a more gradual political approach. REUTERS/Adama Diarra (MALI - Tags: POLITICS)
Mkutano kuhusu MaliPicha: Reuters

"Hatupaswi kupoteza hata sekunde moja. Hii ni dharura, hizi ni mbio dhidi ya wakati," Traore amesema katika hotuba kwa maafisa wa nchi za kigeni.

Washiriki wa mkutano huo baadaye walitoa taarifa ikisema kuwa mkutano huo umewapatia viongozi wa dunia, fursa ya kuungana katika mshikamano na watu wa Mali na kukubaliana , na serikali ya Mali, juu ya mpango wa kuchukua hatua , na kurejesha utaratibu wa katiba, umoja wa kitaifa na ardhi ya Mali.

Dioncounda Traore, Mali's parliamentary head who was forced into exile after last month's coup, is seen after arriving at the airport to take up his constitutionally-mandated post as interim president, in Bamako, Mali Saturday, April 7, 2012. Traore's return comes after coup leader Capt. Amadou Haya Sanogo signed an accord late Friday, agreeing to return the nation to constitutional rule.(Foto:Harouna Traore/AP/dapd)
rais Dioncounda Traore wa MaliPicha: AP

Wameongeza kuwa mkutano huo, umeonesha ishara ya muungano wa Mali, katika diplomasia ya kimataifa.

Baraza la usalama

Mkutano huo umekuja wiki moja baada ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kuidhinisha azimio linalotoa kwa mataifa ya Afrika magharibi siku 45 kupanga mikakati yao kwa ajili ya kuingilia kijeshi katika eneo la kaskazini la Mali.

Eneo hilo kubwa likiwa karibu sawa na nchi ya ufaransa liliangukia mikononi mwa makundi yenye itikadi kali ya dini ya Kiislamu katika mtafaruku ambao ulifuatia mapinduzi ya mwezi Machi mwaka huu nchini humo, nchi ambayo ilikuwa inatambuliwa kama yenye demokrasia imara kabisa katika bara la Afrika.

Wasi wasi kuwa eneo hilo linaweza kuwa maficho ya Waislamu wenye itikadi kali wa kundi la al-Qaeda kama ilivyokuwa Afghanistan muongo mmoja uliopita, majirani wa Mali pamoja na mataifa ya magharibi wana nia kuyaondoa makundi hayo yenye itikadi kali kutoka eneo hilo.

Katika miezi ambayo Waislamu hao wenye itikadi kali wamekuwa katika udhibiti wa eneo hilo, wameweka sheria zao kali za Kiislamu, Sharia, wakiwakamata wanawake ambao hawakujifunika , kuwapiga mawe hadi kufa watu wanaoishi pamoja bila ndoa na kuwakata viungo vya mwili watuhumiwa wa wizi, kwa mujibu wa wakaazi pamoja na makundi ya haki za binadamu.

Maeneo ya kale

Pia wameharibu maeneo ya kale yanayoheshimiwa na Waislamu, maeneo ambayo yamekuwa yakiheshimiwa kwa karne kadha na yamekuwa katika hadhi ya turathi za dunia, lakini Waislamu hao wenye itikadi kali wanayaona kama maeneo ya kukufuru.

Kiongozi wa Mali ameishukuru jumuiya ya kimataifa , na hususan umoja wa Afrika, umoja wa mataifa na mkoloni wa zamani Ufaransa, kwa kuiunga mkono nchini hiyo tangu kuzuka kwa mzozo huo.

South African Home Affairs Minister Nkosazana Dlamini-Zuma addresses the media during the leaders meeting at the African Union (AU) in Addis Ababa July 15, 2012. African leaders brought together the presidents of feuding neighbours Sudan and South Sudan on Saturday and fleshed out a plan for military intervention in northern Mali where they said al Qaeda-linked rebels threatened the continent's security. REUTERS/Tiksa Negeri (ETHIOPIA - Tags: SOCIETY POLITICS)
Rais wa halmashauri ya Afrika Nkosazana Dlamini-ZumaPicha: Reuters

Jumuiya ya uchumi ya mataifa ya Afrika magharibi ECOWAS imesema kuwa inaweza kutuma hadi wanajeshi 3,000 katika hatua ya kulikamata eneo la kaskazini.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na rais mpya wa halmashauri kuu ya umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini - Zuma na rais Goodluck Jonathan wa Nigeria.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe

Mhariri : Bruce Amani