1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMisri

Rais wa Misri aanza ziara nchini India

Bruce Amani
24 Januari 2023

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi anaanza ziara nchini India kesho ambapo atakutana na viongozi wa kibiashara na kuwa mgeni wa heshima katika sherehe za Siku Kuu ya Jamhuri mnamo Januari 26.

https://p.dw.com/p/4Md3I
Ägyptien Präsident Abdel Fattah al-Sisi
Picha: Costas Baltas/AP Photo/picture alliance

Ziara hiyo itajumuisha mazungumzo ya kuimarisha mahusiano ya kiuchumi kati ya nchi hizo mbili na kutafuta fursa za uwekezaji wa India nchini Misri.

Misri inajaribu kuhimiza uwekezaji wa kigeni wakati ikijaribu kushughulikia uhaba wa sarafu ya dola ambayo imesababisha kushuka kabisa kwa pauni ya Misri.

Mwaka jana, ilitafuta msaada kutoka kwa washirika wa Ghuba wenye utajiri wa nishati na shirika la fedha la kimataifa - IMFbaada ya tatizo ka kiuchumi kutokana na vita vya nchini Ukraine kufanya mambo nchini humo kuwa mabaya hata zaidi.