1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ujerumani ahimiza demokrasia na mshikamano

24 Desemba 2023

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ametoa wito kwa raia kulinda demokrasia na kuhimiza ushirikiano katika makundi yote ndani ya nchi ikiwemo vijana.

https://p.dw.com/p/4aXZ4
Ujerumani | Rais Frank-Walter Steinmeier
Rais wa Ujerumani Frank-Walter SteinmeierPicha: Britta Pedersen/dpa-Pol/picture alliance

Katika salamu zake kuelekea sikukuu ya krisimasi na mwaka mpya, Steinmeieramesema ingawa watu wanataka uwazi ni jukumu la walio na dhamana za uwajibikaji katika siasa kutafuta majibu ambayo yataleta mwangaza kwa taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Ulaya.

Wito wa kiongozi huyo inakuja huku kukiwa na ongezeko la uungwaji mkono wa siasa kali za upande wa mrengo wa kulia nchini humo huku ukosoaji wa utendaji wa serikali ukiongezeka. 

Soma pia:Rais wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier amesema Ujerumani itasimama na Israel katika vita vyake Ukanda wa Gaza

Aidha kiongozi huyo amehimiza ushirikishwaji wa makundi yote katika kujenga mustakabali wa Ujerumani, ikiwemo vijana na wahamiaji ambao wanaishi Ujerumani.