1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ujerumani ziarani Rwanda

7 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D3gd

KIGALI:

Rais wa Ujerumani Horst Köhler alie ziarani nchini Rwanda amesema mataifa duniani yapaswa kujifunza kutokana na mauaji ya halaiki yaliotokea Rwanda miaka 14 iliyopita.Köhler alitembelea jumba la ukumbusho katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali ambako kuna maonyesho ya yale yaliyotokea wakati wa mauaji hayo.Baadae Rais Köhler alisema,kilichotokea nchini Rwanda ni kidonda katika historia ya nchi hiyo na ulimwengu mzima.Si chini ya watu 800,000 waliuawa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda katika mwaka 1994.Vile vile takriban watu milioni mbili walikimbilia nchi za jirani.

Rwanda ni kituo cha pili na mwisho katika ziara ya Rais Köhler barani Afrika, iliyoanzia Uganda.Baada ya kukutana na Rais Paul Kagame wa Rwanda,Rais Köhler aliekuwa mkurugenzi mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF,alitoa mwito wa kuwepo uhusiano wa biashara wa haki.Amesema,huo ni msingi muhimu kupiga vita umasikini barani Afrika.