1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Uturuki na Japan zazungumzia mkataba wa Bahari Nyeusi

Tatu Karema
9 Septemba 2023

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amefanya mazungumzo na waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida kuhusu kufufua mkataba wa usafirishaji wa nafaka kupitia Bahari Nyeusi

https://p.dw.com/p/4W8ma
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akihutubia wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri mjini Ankara mnamo Septemba 5, 2023
Rais wa Uturuki Recep Tayyip ErdoganPicha: Mustafa Kamaci/AA/picture alliance

Mapema mwezi huu, Erdogan alisema kuwa, baada ya majadiliano yake na Rais wa Urusi Vladimir Putin, kuna uwezekano wa kuufufua mkataba huo wa nafaka.

Urusi ilijiondoa katika mkataba wa usafirishaji nafaka 

Urusi ilijiondoa katika mkataba huo uliokuwa ukisimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki kutokana na malalamiko kuwa usafirishaji wa bidhaa zake za vyakula na mbolea ulikuwa ukikabiliwa na vikwazo. Ilisema pia kwamba nafaka za Ukraine hazikuwa zikipelekwa katika nchi zenye uhitaji.