1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Tofauti kati ya rais Abbas na chama cha Hamas zazidi

18 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1W

Mzozo kati ya chama tawala cha Hamas nchini Palestina na rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, umechukua mueleko mpya leo baada ya rais Abbas kupendekeza kuundwe baraza la mawaziri la mpito litakalojumuisha wasomi badala ya wanasiasa.

Abbas amependekeza kuundwe serikali ya wasomi baada ya juhudi za kuunda serikali ya umoja wa taifa kugonga mwamba.

´Serikali ya wasomi haitakuwa na jukumu kwa kundi lolote katika utendaji wake. Makundi mengi na mashirika mbalimbali ya kijamii pamoja na viongozi wa vyama vyote viwili vya kisiasa wanasema serikali hii inawezekana kwa kipindi cha mwezi mmoja, miezi sita na hata mwaka mmoja, lakini muda uwe chini ya mwaka. Baadaye tutaona mambo yatakavyokwenda. Angalao tunaweza kujikwamua kutokana na tatizo linalotukabili.´

Msemaji wa chama cha Hamas, Ghazi Hamad, amelitupilia mbali pendekezo la rais Abbas akisisitiza wanataka serikali itakayowajumuisha wanasiasa na wasomi.