1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH. Wasiwasi wa Marekani kuhusu Abbas na serikali mpya

17 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRH

Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas leo amekutana na mjumbe wa Marekani wa ngazi ya juu mjini Ramallah.Marekani ina wasiwasi kuhusu msaada wa Abbas kuhusika na kuundwa kwa serikali ya mseto, kati ya chama cha Hamas chenye msimamo mkali na chama chake cha Fatah kinachofuata siasa za wastani.Kwa mujibu wa washauri wa Rais Abbas,maafisa wa Kimarekani wamemuambia Abbas kuwa wataisusa serikali yo yote ya Wapalestina itakayokataa kuitambua Israel.Rais Abbas alikubali kugawana madaraka na chama cha Hamas kwa matumaini ya kukomesha mapigano makali ya miezi kadhaa kati ya Hamas na Fatah,licha ya kuwepo uwezekano kuwa mradi wa serikali mpya hautoiridhisha jumuiya ya kimataifa au kusaidia kuondosha vikwazo vya msaada vinavyowaumiza Wapalestina.