1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RANGOON: Utawala wa kijeshi hautaki kujadiliana na upinzani

13 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7GC

Utawala wa kijeshi nchini Burma umekataa mwito wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,kujadiliana na upinzani unaogombea demokrasia.Stesheni ya televisheni ya taifa imesema,utawala huo umesikitishwa na taarifa ya Baraza la Usalama, iliyokosoa utumiaji wa nguvu katika ukandamizaji wa maandamano ya amani hivi karibuni,nchini Burma.Imesema wito wa Baraza la Usalama, kuachilia huru wafungwa wa kisiasa na waandamanaji waliotiwa ndani,hauakisi matakwa ya umma wa Burma.Wakati huo huo,serikali ya kijeshi imesisitiza kuwa ipo tayari kufanya kazi na Umoja wa Mataifa,lakini itafuata njia yake kuhusu demokrasia.