1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIGA: Vingozi wa nchi nane za umoja wa ulaya wakamilisha mkutano

11 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAk

Marais wanane wa nchi za umoja wa ulaya wamekamilisha mkutano wao katika mji mkuu wa Riga nchini Latvia.

Kikao hicho kilizingitia maswala ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuhusu marekebisho ya katiba ya umoja wa ulaya.

Rais Heinz Fischer wa Austria amesisitiza makubaliano ya katiba ambayo yamekwama kuafikiwa tangu wapiga kura wa Ufaransa na Uholanzi kupinga katika kura ya maoni ya mwaka 2005.

Marais kutoka Austria, Finland Ujerumani, Hungary, Italia, Latvia, Poland na Portugal walihudhurila kikao hicho.