1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya Wikileaks juu ya Unyanyasaji Iraq.

Halima Nyanza23 Oktoba 2010

Marekani imeelezwa kwamba ilitambua, lakini ilishindwa kuchunguza matukio ya kuwanyanyasa wafungwa nchini Iraq.

https://p.dw.com/p/Plse
Mtandao wa Wikileaks, unaotoa ripoti kuhusiana na kunyanyaswa kwa wafungwa nchini Iraq.Picha: picture alliance/dpa

Marekani ilitambua lakini ilishindwa kuchunguza visa vya unyanyasaji wa wafungwa kulikofanywa na  maafisa wa usalama wa Iraq.

Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari kuhusu nyaraka laki nne zilizofichuliwa kuhusu vita vya Iraq.

WikiLeaks / Irak / Ausschnitt Screenshot / NO-FLASH
Kurasa ya mtandao wa WikiLeaks kama ulivyoonekana jana Ijumaa, ambapo ulitoa nyaraka 391,831 za kuanzia 2004 hadi Jan. 1, 2010, juu ya unyanyasaji unaofanywa na wanajeshi wa Iraq dhidi ya wafungwa.

Mtandao wa wikileaks umetoa nyaraka hizo kwa vyombo kadhaa vya habari  hapo jana usiku likiwemo gazeti la Ujerumani la Der Spiegel.

Nyaraka hizo zinaonekana kuonyesha kuwa mamia ya raia wa Iraq waliuawa na wanajeshi wa Marekani katika vizuizi tangu kuvamiwa kwa nchi hiyo mwaka 2003.

Hata hivyo Marekani imekosoa kufichuliwa kwa kiasi kikubwa kwa taarifa hizo kuliko ilivyokuwa awali na kusema  kuwa uhalifu wowote uliojulikana uliripotiwa kwa maafisa husika.