1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH: Mwito kwa Musharraf kuondoka madarakani

5 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79q

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz Sharif ametoa mwito kwa Rais Pervez Musharraf kujiuzulu moja kwa moja.Wakati huo huo ameiomba jumuiya ya kimataifa ilaani vikali amri ya hali ya hatari iliyotangazwa na Musharraf.

Akizungumza Saudi Arabia anakoishi uhamishoni, Sharif amesema,Musharraf akiendelea kubakia madarakani,Pakistan itatumbukia katika janga la vurugu.Akaongezea,

„Musharraf ameichukua hatua hiyo kwa sababu za kibinafsi.Mtu mmoja ameiteka nyara nchi nzima kwa maslahi yake mwenyewe. Ametaka urais kwa awamu nyingine na labda uamuzi wa Mahakama Kuu ya Pakistan,uliokuwa ukingojewa ungempinga.Kwa hivyo amechukua hatua kali dhidi ya mahakama na jamii nzima ya raia wa Pakistan.“

Kwa mujibu wa ripoti rasmi,saa 24 baada ya kutangazwa kwa hali ya hatari,kiasi ya wapinzani 500 wametiwa ndani.Vile vile,uchaguzi uliopangwa kufanywa Januari ijayo,sasa umeahirishwa kwa muda usiojulikana.