1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Roberto Di Matteo ndiye kocha mpya wa Schalke

7 Oktoba 2014

Aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Roberto Di Matteo amepewa jukumu la kuifunza klabu ya Schalke. Hii ni baada ya Jens Keller kutimuliwa kama kocha wa klabu hiyo ya Ujerumani kutokana na mwanzo mbaya wa msimu

https://p.dw.com/p/1DROO
ARCHIV Roberto Di Matteo italienischer Interimstrainer von FC-Chelsea
Picha: AP

Keller ametimuliwa baada ya kuwa na mwanzo mbaya msimu huu ambapo Schalke imepata tz points nane pekee katika mechi saba za lifi ya Bundesliga. Kwa sasa vijana hao wa jimbo la Gelsenkirchen wako katika nafasi ya 11 kati ya timu 18 za ligi hiyo kuu ya Ujerumani.

Ilishindwa magoli mawili kwa moja na Hoffenheim mwishoni mwa wiki na pia wameondolewa katika Kombe la Shirikisho la Soka la Ujerumani – DFB na klabu ya daraja la tatu Dynamo Dresden.

Keller mwenye umri wa miaka 43 amekuwa kocha wa Schalke tangu Desemba 2012 lakini amekuwa akikabiliwa na mbinyo wa kutokana na matokeo yasiyoridhisha.

Di Matteo ambaye alikuwa kiungo wa timu ya Italia aliiongoza Chelsea katika kushinda Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka wa 2012, kwa kuipiku Bayern Munich katika uwanja wake wa Allianz Arena nchini Ujerumani. Lakini akafutwa kazi msimu uliofuata.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Sekione Kitojo