1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Roketi zimepiga uwanja wa ndege wa Libya mjini Tripoli

Josephat Charo
20 Aprili 2018

Msemaji wa kikosi maalumu kinacholinda usalama katika uwanja huo wa kijeshi wa Mitiga, Rada, amesema kombora moja liliipiga ndege aina ya Airbus 320 na mengine yakaupiga ukumbi wa abiria wanaowasili katika uwanja huo.

https://p.dw.com/p/2wNqJ
Libyen Flughafen Tripolis Mitiga
Picha: Reuters

Roketi zimepiga uwanja mkubwa wa ndege wa Libya mjini Tripoli na kuiharibu ndege ya abiria iliyokuwa ikisubiri kupaa mapema jana.

Msemaji wa kikosi maalumu kinacholinda usalama katika uwanja huo wa kijeshi wa Mitiga, Rada, amesema kombora moja liliipiga ndege aina ya Airbus 320 na mengine yakaupiga ukumbi wa abiria wanaowasili katika uwanja huo lakini hakuna aliyeruhiwa.

Hujuma hiyo ilifanywa siku ambayo mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya, Ghassan Salame, na balozi wa Ufaransa nchini Libya, Brigitte Curmi, walipowasili katika uwanja huo wa ndege, ambao pekee ndio unaofanya kazi mjini Tripoli.

Afisi za maafisa hao hazikutoa taarifa mara moja kuhusu shambulizi hilo. Curmi na Salame walikutana na wajumbe wa serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa kujadili kuhusu uchaguzi.