1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROMA: Waziri mkuu wa Italia Romano Prodi ajiuzulu

22 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPn

Waziri mkuu wa Italia, Romano Prodi, amejiuzulu kufuatia kikao cha dharura cha baraza la mawaziri mjini Roma. Prodi alijiuzulu saa chache baada ya serikali yake ya mrengo wa kati na kushoto kushindwa kwa idadi ndogo ya kura katika bunge.

Kura iliyopigwa bungeni ilihusu sera ya Italia kuelekea mataifa ya kigeni. Sera hiyo ilijumulisha mpango wa kurefusha muda wa wanajeshi 2,000 wa Italia walio nchini Afghanistan na kuidhinishwa kwa upanuzi wa kambi ya jeshi la Marekani katika mji wa kaskazini wa Vicenza.

Haijabainika wazi ikiwa rais wa Italia, Giorgio Napolitano, atakubali kujiuzulu kwa serikali ya waziri mkuu Romano Prodi.

Rais Napolitano ameitaka serikali ya bwana Prodi iendelee kuitawala Italia mpaka atakapopitisha uamuzi.