1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME:Jumuiya ya kimataifa yatoa mwito kusaidiwa Afghanstan

4 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlx

Wafadhili wa kimataifa wametoa wito wa kutolewa euro millioni 360 kuisadia Afghanstan kuweka mfumo mpya wa sheria.

Katika mkutano uliofanyika mjini Rome Italia rais wa Afghanstan Hamid Karzai amesema mfumo wa sheria nchini mwake utasalia kuwa kitendawili mradi ugaidi unaendelea kufanyika takriban kila siku. Wakati huo huo katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO Jaap De Hoop Scheffer ametoa wito pafanyike uchunguzi wa mauaji ya raia nchini Afghanstan.

Aliongeza kusema jamii ya Afghanstan lakini isisahau kwamba NATO haina dhamira ya kuendesha mauaji ya raia kwa makusudi. Rais Karzai pia ameongeza kusema mageuzi ya demokrasia yatachukua muda katika nchi hiyo inayokabiliwa na vitisho vya magaidi baada ya kung’olewa madarakani kwa utawala wa Taliban.