1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ronaldo: fainali iwe kati ya Brazil na Ujerumani

6 Juni 2014

Homa ya kombe la dunia nchini Brazil litakalofungua dimba tarehe 12 ya mwezi huu imeanza na mchezaji wa zamani wa Brazil Ronaldo anasema anaamini fainali tarehe 13 Julai itakuwa kati ya Ujerumani na Brazil.

https://p.dw.com/p/1CDvf
Ronaldo Fußballspieler 2002
Picha: Patrick Hertzog/AFP/Getty Images

Ronaldo aliyekuwa mshambuliaji nyota wa brazil anasema anaamini fainali itakuwa ni marudiano ya pambano kati ya Ujerumani na Brazil kule Korea kusini 2002 ambapo Brazil ilishinda mabao 2-0 na kulinyakuwa kombe hilo. Mashindano hayo utakumbhuka yaliandaliwa kwa ubia kati ya Korea kusini na Japan.

Ronaldo alisema anasubiri kwa hamu kujionea fainali hiyo katika uwanja wa maracana mwezi ujao. Katika mahojiano na Shirika la habari la Ujerumani DPA katika ukurasa wake maalum kuhusu kombe la dunia, Ronaldo pia aliwataja Cristiano Ronaldo wa Ureno, Mfaransa Frank ribery , Mbrazil Neymar na thomas muller wa Ujerumani kuwa wachezaji watakaotokeza kuwa nyota katika mashindano hayo. Akiulizwa kuwa mechi anazotarajia kuwa ngumu, Ronaldo alizitaja uhispania dhidi ya Uholanzi, Ureno na ujerumani na pambano kati ya Uingereza na Italia.

Bildergalerie Iran Fussball Team in Sao Paulo Brasilien WM 2014
Vijana wa Brazil wakipasha misuli moto katika kambi yao ya mazoezi mjini Sao Paolo, BrazilPicha: Miguel Schincariol/AFP/Getty Images

kwa upande mwengine, kihistoria kila mara Brazil ilipolitwaa kombe la dunia, basi aliyelinyanyuwa kwanza alikuwa ni mshambuliaji. Hivi sasa nyota na mshambuliaji Neymar ana ndoto hiyo. Mwenyewe anaungama kwamba haitokuwa rahisi kufuata nyayo za wachezaji kama Pele na Garrincha au Ronaldo walioongoza Brazil kulitwaa kombe la dunia , lakini kijana Neymar mwenye umri wa miaka 22 na mchezaji wa timu ya Barcelona ya Uhispania ana matumaini mafanikioo hayo yatafikiwa katika mashindano haya ya mwezi huu hadi ujao wa Julai.

Deutsche Fußballnationalmannschaft Training
Kikosi cha Ujerumani kina matumaini ya kutwaa Kombe la Dunia kwa mara ya nnePicha: Getty Images/Martin Rose

Katika kilabu yake ya Barcelona amefunga mabao 11 katika mechi 15 alizoichezea Brazil na magoli 30 katika mechi 47 za kimataifa . Mchezaji wa zamani Cafu anasema Neymar ni mtu muhimu katika ngazi ya ushambuliaji ya kikosi cha Brazil. Brazil ndiyo itakayofungua dimba la mashindano hayo ya Kombe la dunia hapo Juni 12 itakapochuana na Kroatia.

Wakati huo huo Shirikish la kandanda la kimataifa FIFA limetoa orodha mpya ya ubora wa timu za taifa za kandanda . Katika orodha hiyo Brazil imechupa hadi nafasi ya tatu kutoka ya nne. nafasi ya Kwanza ni uhispania ikiifuatiwa na Ujerumani. hivi sasa nafasi ya nne ni ureno. Kwa upande wa nchi ztano za Afrika katika mashindano hayo ya kombe la dunia safari hii, Algeria iko nafasi ya 22, ifuatiwa na cote d´ivoire 23, nafasi ya 37 ni Ghana . Nigeria iko nafasi ya 44, Cameroun, hamsini na sita. Wakati huo huo habari za kuskitisha kwa ghana na Afrika ni kuwa mlinzi wa kati wa timu ya taifa ya Ghana , Jerry Akaminko atayakosa mashindano hayo baada ya kuumia kisigino cha mguu wa kushoto katika pambano la kirafiki dhidi ya Uholanzi Jumamosi iliopita.

Mwandishi : Mohammed Abdul-Rahman
Mhariri. saumu Yusuf