1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROSTOCK:Mahakama Ujerumani yaridhia udhibiti wa waandamanaji

5 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBub

Mahakama ya katiba ya Ujerumani imeridhia udhibiti wa wandamanaji dhidi ya mkutano wa wakuu wa nchi za G8 hapo kesho huko Heilegindamm.

Mahakama hiyo imesema kuwa ni watu 15 tu wawakilishi wa wapinzani wa utandawazi watakaoruhusiwa kukesha hii leo katika eneo la hoteli kutakakofanyika mkutano huo.

Mapema ghasia ziliendelea za waandamanaji ambapo kiasi cha polisi 50 walijeruhiwa na waandamanaji 66 walikamatwa.