1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda: Mamlaka ya Magereza yaitaka serikali iwaachie wafungwa wazee

4 Mei 2012

Mamlaka ya magereza nchini Rwanda yameitaka serikali ya nchi hiyo kuwaachia wafungwa zaidi ya 2000 ambao wanakabiliwa na tatizo la uzee linalowasababishia kupoteza maisha yao kutokana na maradhi.

https://p.dw.com/p/14pW7
Wazee Wakongwe wanapoteza maisha kwenye magereza ya Rwanda
Wazee Wakongwe wanapoteza maisha kwenye magereza ya RwandaPicha: Fotolia/rudall30

Mamlaka hiyo imesema zaidi ya asilimia 60 ya mahabusu wanaopoteza maisha kwenye magereza ya Rwanda ni wazee wakongwe wenye umri zaidi ya 70. Mamlaka ya magereza yanasema kwamba mwito unawahusu hata mahabusu wa mauaji ya kimbari ya mwaka 94 nchini Rwanda.

Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi.

(Kusikiliza ripoti bonyeza alama ya spika za masikioni)

Mwandishi: Sylvanus Kalemera

Mhariri: Othman Miraji