1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Simba warudi Rwanda

7 Julai 2015

Rwanda imewarudisha simba katika mbuga yake ya Kitaifa ya Akagera kutoka nchini Afrika Kusini baada ya Simba wa mwisho kuonekana katika mbuga hiyo mwaka 2006.

https://p.dw.com/p/1FtzI
Bildergalerie Asiatischer Löwe
Picha: picture alliance / blickwinkel/D. & M. Sheldon

Rwanda pia ina mipango ya kuongeza faru katika mbuga yake katika kipindi cha mwaka mmoja wakati nchi hiyo ikijaribu kuwavutia watalii zaidi.

Kwa mujibu wa afisa mmoja katika mbuga hiyo shughuli za kuwatembeza watalii katika kile kinachoitwa safari ni biashara maarufu zaidi katika eneo la Afrika Mashariki na wanyama watano wakubwa wenye umaarufu barani Afrika ambao wanajumuisha Simba na Faru ndio kivutio kikubwa kwa watalii wanaokwenda katika Safari.

Tayari mbuga ya Akagera inao Chui,Nyati na Ndovu ambao ni miongoni mwa wanyama watano wakubwa wenye umaarufu kwa watalii.

Nchi ya Rwanda, bado inategemea misaada baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 baada ya kuligawa taifa hilo, inayojulikana sana kwa safari ya kwenda kuwaona sokwe walio hatarini kutoweka waliopo kwenye mteremko wa milima ya Virunga, lakini nchi hiyo imejaribu kuimarisha utalii ili kuongeza mapato.

Tumewarudisha simba wanne kati ya watano wakubwa Jes Gruner, meneja wa mbuga ya taifa ya Akagera, aliwaambia waandishi wa habari baada ya simba waliokuwa wakihamishwa kutoka mbuga mbili nchini Afrika Kusini kufika nchini Rwanda.

BdT Deutschland Gorilla Fatou
Picha: picture-alliance/dpa/P. Zinken

Simba Majike watano na madume wawili walisafirishwa kutoka kwenye hifadhi ndogo mbili za Afrika ya kusini , ambapo mara kwa mara waliibua hoja ya kuwaondoa wanyama hao ili kuepuka kuzaliana zaidi. Wanyama hao saba walichaguliwa ili kukuza kizazi chao.

Moja ya changamoto kubwa zizoikabili kila mbuga au eneo la uhifadhi ambalo linatunza Faru ni kuhakikisha kuna kuwa na ulinzi wa kutosha wa kuzuia majangili,ambao wanatafuta pembe kwa ajili ya kuziuza kwa wanunuzi wa Asia.

Mbuga ya Akagera inatumika kama makazi ya simba, lakini simba wa mwisho alipewa sumu na wamiliki wa ng'ombe, ambaye alikuwa akiishi katika Hifadhi baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, watu 800,000 waliuawa. Simba wa mwisho alionekana mwaka 2006.

Sokwe bado ni kivutio kikuu cha utalii nchini Rwanda na moja ya chanzo kikubwa cha mapato ya utalii, kwa kila mtu mmoja kulipa dola mia moja kwa ajili ya safari fupi kuwaona wanyama hao,ikijumuisha gharama za usafiri na malazi .

Lakini mbuga ya Akagera inawavutia wageni wengi zaidi ya mbuga nyingine nchini Rwanda, na wageni 28,000 walitembela mbuga hiyo mwaka jana.

Rwanda imekuwa na ushindani wa kikanda katika kile kinachojulikana kama safari ni biashara na nchi ya Kenya na Tanzania, nchi zote mbili mbali ya kuwa ni kubwa lakini pia zimejiimarisha katika sekta ya utalii, lakini sekta ya utalii nchini Kenya imekuwa ikisuwa suwa kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo kutokana na mashambulizi ya Kiislam.

Mhandishi:Salma Mkalibala/RTRE

Mhariri:Iddi Ssessanga