1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SADC inaadhimisha miaka 25 tangu ilipoanzishwa

Zainab Aziz
17 Agosti 2017

Uhasama wa kisiasa na tofauti za kiuchumi ni mambo yanayoigubika jumuia ya ushirikiano na maendeleo kusini mwa Afrika SADC. Jumuia hiyo inaadhimisha miaka 25 hivi sasa tangu ilipoanzishwa.

https://p.dw.com/p/2iO4Q
Afrika SADC Gipfel in Mozambik, Maputo
Picha: AFP/GettyImages

Serikali ya Afrika Kusini inajiandaa kukabidhiwa wadhifa wa juu; Wiki hii nchi hiyo ya ras ya matumaini mema itakadhibiwa wadhifa wa mwenyekiti wa jumuia ya ushirikiano na maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC.Katika mkutano wa kilele Agosti 19 inayokuja mjini Pretoria, rais wa Afrika kusini Jacob Zuma atakabidhiwa wadhifa huo kutoka kwa mfalme Mswati III wa Swaziland.Mataifa madogo hasa miongoni mwa ataida 15 wanachama wa SADC ndiyo yanaayotarajiwa kuangalia kwa jicho loa wasi wasi wadhifa wa Afrika Kusini kama mwenyekiti wa jumuia hiyo ya kimkoa. "Nafasi ya Afrika kusini katika kanda hiyo inaangaliwa kwa jicho la wasi wasi. Nchi hiyo daima aimekuwa ikijiangalia kuwa asawa na kaka mkubwa na kujiweka kando ili isiwakanyage wengine" Anasema Talitha Berthelsmann-Scott, ambae ni mtumishi wa taasisi ya masuala ya kimataifa nchini Afrika Kusini-SAIIA.

Swaziland König Mswati III und Inkhosikati LaMbikiza
Mwenyekiti wa SADC Mfalme Mswati wa Swaziland Picha: Getty Images/AFP/K. Sahib

Malengo ya jumuia ya hiyo ya mataifa ya kusini mwa Afrika ni makubwa: utulivu wa kisiasa,na autawala bora utakaochochewa kutokana na maendeleo ya kiuchumi na biashara. Mnamo mwaka 2008 kwa hivyo mataifa ya jumuia ya SADC yakatiliana saini makubaliano ya biashara huru. Lakini mengine hayajajiunga na makubaliano hayo na hakuna maendeleo ya maana yaliyoweza kupatikana katika ushirikiano wa kiuchumi wa mataifa hayo, anasema Bertelsmann-Scott katika mahojiano na DW.Na hali hiyo haitobadilika hata kama Afrika Kusini ndio itakayokabidhiwa wadhifa wa mwenyekiti wa jumuia hiyo, anasema. Afrika Kusini haijawahi kuwa tayari kujiunga na umoja mpana wa forodjha badala yake imejiunga na umoja wa forodha pamoja na mataifa ya Swaziland, Botswana, Leostho na Namibia ambayo pia ni wanachama wa SADC.

Simbabwe Wahlen Juli 2013
SADC pia inahusika katika uangalizi wa uchaguziPicha: Jekesai Njikizana/AFP/Getty Images

wanachama wa SADC wanashindwa kukubaliana kama kanda yao ianzishe kwanza viwanda na kuimarisha miundo mbinu au la,anasema mtaalam huyo. Na hilo hasa ndilo serikali ya rais Zuma inalotaka kuliishadidia na baadae kuwekeza katika sekta za jadi mfaano wa migodi,viwanda vya madawa na sekta ya huduma za jamii. Soko la pamoja na nishati liko tayari na mipaka ya mbuga za wanyama pia imeshaondoshwa kwa namna ambayo watalii wakipata viza moja wanaweza kuzitembelea mbuga za wanyama za nchi zote wanachama.Hata hivyo bado kuna tatizo nalo ni kwamba mataifa wanachama wa SADC badala ya kushirikiana wenyewe kwa wenyewe,wanashirikiana kwa nguvu pamoja na Chna, India au Brazil au na madola ya zamani ya ukoloni.

Miaka 25 tangu ilipoundwa,jumuia ya aushirikiano na maendeleo kusini mwa Afrika SADC, licha ya kwamba malengo iliyojiwekea ni makubwa hata hivyo hatua za maana zimeweza kufikiwa,ukuaji wa kiuchumi ni mkubwa bila ya kusahau makubaliano ya kibiashara yaliyofikiwa kati ya baadhi ya mataifa ya SADC na Umoja wa ulaya mwaka 2016. Kuna dhamiri ya kuimarisha ushirikiano anasema Matthias Boddenberg, ambae ni mkuu wa baraza la biashara na viwanda la Ujerumani kwa eneo la kusini mwa Afrika.

Mwandishi: Martina Schwikowski/Hamidou Oummilkheir
Mhariri: Mohammed Khelef