1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Samara, Russia. Russia na umoja wa Ulaya waonyeshana umwamba.

19 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0m

Mkutano baina ya umoja wa Ulaya na Russia umemalizika kwa utata kwa viongozi wa umoja huo na rais Vladimir Putin kuvutana kuhusiana na suala la uhuru wa kidemokrasia.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa vikwazo vya kusafiri dhidi ya wapinzani wa serikali ya Russia, ikiwa ni pamoja na bingwa wa zamani wa mchezo wa Chess Garry Kasparov vimevuka mpaka.

Putin amesema kuwa vikwazo hivyo ni hatua ya usalama , akiifananisha na juhudi kama hizo zinazofanyika katika bara la Ulaya.

Rais wa Russia amekosoa jinsi wanavyofanyiwa watu wenye asili ya Russia katika mataifa wanachama wa umoja wa Ulaya ya Latvia na Estonia.

Amewashutumu maafisa wa Estonia kwa kuhusika na kifo cha raia wa Russia katika ghasia mwezi uliopita ambazo zilizuka baada ya Estonia kuliondoa sanamu la kumbukumbu ya enzi za vita katika utawala wa Urusi ya zamani. Rais wa halmashauri ya Ulaya Jose Manuel Barosso amesema kuwa tatizo litakaloikumba Estonia litakuwa tatizo la umoja wa Ulaya.