1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

San Francisco: Wakaazi katika wilaya tano za California wanatakiwa wabakie majumbani kutokana na hewa chafu iliosababishwa na moto uliotokea.

28 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7C3

Huko Marekani, wakaazi walioathirika na moto uliotokea katika mkoa wa California wameonywa juu ya hewa chafu.

Wakaazi katika wilaya tano za kusini za mkoa huo wamehimizwa wabakie majumbani kwa vile uchafu wa hewa umezidi mara tatu ya kima cha kawaida. Si chini ya watu 14 wamekufa kutokana na moto uliotokea katika mkoa huo hivi karibuni.