1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANTIAGO DE CHILE: Pinochet anachukua dhima ya kisiasa

26 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpI

Dikteta wa zamani wa Chile,Augusto Pinochet amesema,anakubali kile alichokiita „dhima ya kisiasa“ kuhusika na yale yaliyotokea baada ya mapinduzi yake ya kijeshi ya mwaka 1973.Katika barua iliyosomwa na mke wake,siku ya kutimiza miaka 91 tangu kuzaliwa kwa Pinochet,dikteta huyo wa zamani amesema,utiifu wake kwa taifa ulichochea vitendo vyake vyote.Wakati wa utawala wa Pinochet,kufuatia mapinduzi yaliyomngóa madarakani rais Salvador Allende,kiasi ya watu 3,000 waliuawa au walitoweka na kama 28,000 wengine waliteswa.