1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANTIAGO : Fujimori kurudishwa Peru kujibu mashtaka

21 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNr

Rais wa zamani wa Peru Alberto Fujimori kurudishwa nyumbani kutoka Chile ili kujibu mashtaka ya rushwa na ukiukaji wa haki za binaadamu wakati wa utawala wake mwaka 1990 hadi mwaka 2000.

Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa mahkama kuu ya Chile hii leo ambao hauwezi kubatilishwa na hiyo Fujimori atarudishwa nyumbani baada ya kuishi uhamishoni kwa muda wa miaka saba.

Fujimori mwenye umri wa miaka 69 alikimbilia Japani mwaka 2000 kufuatia kashfa ya rushwa na alijiuzulu kwa barua aliyotuma kwa Fax akiwa hotelini mjini Tokyo.

Wakili wa kiongozi huyo wa zamani Gabriel Zalianski amesema mteja wake amekubaliana na uamuzi wa mahkama kurudishwa Chile kujibu mashtaka yanayomkabili.