1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SAO PAULO: Papa Benedict aendelea na ziara yake Brazil.

10 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3Y

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Benedict wa kumi na sita amewasili nchini Brazil kwa ziara ya siku tano.

Hiyo ndiyo ziara ya kwanza ya Papa katika eneo la Amerika Kusini ambako kuna karibu nusu ya idadi ya wafuasi wa kanisa Katoliki duniani.

Papa Benedict anatembelea Brazil kwa nia ya kufungua rasmi kongamano kubwa la maaskofu wa Amerika Kusini siku ya Jumapili katika mji wa Aparecida.

Kongamano hilo linalenga kuandaa mikakati ya kukabiliana na idadi inayoongezeka ya wakatoliki wanaoasi kanisa lao katika eneo hilo na kujiunga na madhehebu ya Kiinjili.

Mara alipowasili mjini Sao Paulo, Papa alitoa hotuba akipinga utoaji mimba akisema maisha ya mwanadamu yanapaswa kuheshimiwa tangu kuzaliwa mpaka kufa kwake.

Papa alisema hayo jana kiasi wiki mbili baada ya Mji wa Mexico City, ambao una wakatoliki wengi, kuruhusu utoaji mimba.