1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia kuanzisha mahusiano upya na Syria

24 Machi 2023

Syria na Saudi Arabia wamekubaliana kufungua upya balozi zao baada ya kukata mahusiano ya kidiplomasia kwa zaidi ya muongo mmoja,

https://p.dw.com/p/4PA2C
Kombobild | Baschar al-Assad und Mohammed bin Salman
Picha: Mikhail Tereshchenko/IMAGO/Rungroj Yongrit/AFP/Getty Images

Taarifa hii ni kulingana na vyanzo vitatu vyenye uelewa na suala hilo. Hatua hiyo inatarajiwa kuifungulia milango Damascus kurejea kwenye muungano wa mataifa ya Kiarabu.

Kasi ya mawasiliano kati ya Riyadh na Damascus imeongezeka baada ya makubaliano ya kihistoria ya kuanzisha upya ushirikiano kati ya Saudi Arabia na Iran, ambayo ni mshirika mkubwa wa rais Bashar al-Assad, kimesema chanzo chenye mafungamano na Damascus.

Soma pia: Assad azilaumu Uturuki,Saudia,na Qatar

Syria ilikuwa imetengwa na mataifa mengi ya Kiarabu na ya magharibi tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoanza nchini humo mwaka 2011.