1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSaudi Arabia

Saudi Arabia yaukaribisha ujumbe wa Iran na Syria

13 Aprili 2023

Saudi Arabia imewapokea wajumbe wa kihistoria kutoka mataifa ya Iran na Syria, wakati nchi za Ghuba zikijiandaa kurejesha uhusiano wao wa kidiplomasia baada ya miaka mingi ya mgawanyiko.

https://p.dw.com/p/4PzBp
Saudi Arabien | Waleed El Khereiji und Faisal Mekdad
Picha: SAUDI PRESS AGENCY/REUTERS

Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imesema waziri wa mambo ya nje wa Syria Faisal Mekdad amekutana na mwenzake wa Saudi Arabia na kujadili kwa kina hatua za kuchukua ili kufikia suluhu kamili ya kisiasa katika mgogoro wa Syria, lengo likiwa ni kupata muafaka wa kitaifa na kulirejesha taifa hilo katika ulimwengu wa Kiarabu.

Soma pia: Ujumbe wa Iran wazuru Saudia kusawazisha mahusiano

Wakati hayo yakijiri Rais wa Iran Ebrahim Raisi anatarajiwa nchini Saudi Arabia hivi karibuni, huku taifa hilo likiendelea na majadiliano na waasi wa Kihouth katika kukomesha mapigano huko Yemen, hatua iliyozidi kuongeza matumaini ya kuleta utulivu katika mataifa ya Ghuba.