1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz ajitayarisha kwa ziara ya China

12 Aprili 2024

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani atakwenda China kwa ziara ya siku tatu itakayotuama juu ya masuala ya biashara, akitumai kuvutia mahusiano ya karibu na Beijing

https://p.dw.com/p/4ehp4
Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Scholz ambaye atafuatana na ujumbe mkubwa wa wafanyabiashara na wakuu wa kampuni za kijerumani, amepangiwa kufanya mazungumzo na Rais Xi Jinping pamoja na maafisa wengine wa ngazi ya juu wa China. 

Anatarajiwa kulizusha suala la umuhimu wa kuwepo usawa katika kulifikia soko la China, jambo ambalo makampuni ya kijerumani yameliliamikia kwa muda mrefu. 

Taiwan yamrai Scholz kuionya China kutotumia mabavu

Ajenda nyingine itakuwa ni uzani wa ushindani kibiashara baada ya nchi nyingi za magharibi kuituhumu China kutoa ruzuku kubwa kwa viwanda vyake kuzalisha  bidhaa kupita kiasi. Hivi sasa Umoja wa Ulaya unalenga kuziwekea vikwazo vya kiushuru bidhaa za China ikiwemo magari ya umeme na paneli za kufua umeme kwa nguvu ya jua na upepo kutokana na madai ya kuuzwa kwa nafuu.