1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz atarajia Bunge la Marekani kuafikiana kuisaidia Kiev

6 Februari 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema ana imani kuwa wabunge wa Marekani wataafikiana kuhusu mpango wa kuipatia Ukraine msaada wa kifedha unaohitajika.

https://p.dw.com/p/4c56E
Kansela Scholz wa Ujerumani akisalimiana na Waziri Mkuu wa Ufaransa Gabriel Attal
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz (kulia) akisalimiana na Waziri Mkuu wa Ufaransa Gabriel Attal mjini Berlin: 05.02.2024Picha: STEFANIE LOOS/AFP

Scholz ameyasema hayo mjini Berlin baada ya mazungumzo na Waziri mkuu mpya wa Ufaransa Gabriel Attal na kusisitiza kuwa Marekani na Ulaya wanatakiwa kwa pamoja kutuma ujumbe ulio wazi kwa rais wa Urusi Vladimir Putin kuwa wataendelea kuisaidia Ukraine, huku akiyahimiza mataifa ya Ulaya kuendelea kuiwekea shinikizo Urusi.

Soma pia: Viongozi wa Umoja wa Ulaya wahimizana juu ya kuongeza misaada kwa Ukraine

Kansela huyo wa Ujerumani ataanza siku ya Alhamisi ziara yake mjini Washington, na anatarajiwa kukutana na rais Joe Biden siku ya Ijumaa.

Katika mkutano wao wa faragha, wabunge wa Republican wameafikiana kuupinga mpango huo unaojumuisha msaada kwa Ukraine, Israel na hatua za kuimarisha usalama katika mipaka ya Marekani.