1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Semenya ataka kugharamikia mapambano yake ya kisheria

Iddi Ssessanga
9 Februari 2024

Bingwa mara mbili wa Michezo ya Olimpiki, Caster Semenya, ameomba kufadhili mapambano yake ya kisheria dhidi ya sheria zinazowataka wanariadha wa kike wenye viwango vikubwa vya homoni ya testosteroni kumeza dawa.

https://p.dw.com/p/4cDdx
Mwanariadha Caster Semenya (RSA)
Mwanariadha wa kimataifa kutoka Afrika Kusini, Caster Semenya.Picha: Christine Olsson/TT/IMAGO

Mwanariadha huyo wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 33 alishinda kesi ya muda mrefu dhidi ya Uswisi katika mahakama hiyo ya kimataifa yenye makao yake makuu mjini Strassbourg, ambayo iliamua kwamba alikuwa muathirika ya ubaguzi.

Soma zaidi: Semenya apeperusha Bendera ya Afrika Kusini Olimpik

Lakini mamlaka za Uswisi, zikiungwa mkono na Shirikisho la Riadha Duniani, zimelipeleka suala hilo katika jopo la juu la mahakama hiyo, ambalo maamuzi yake yana nguvu ya kisheria.

Soma zaidi: Mahakama ya CAS yaanza kusikiliza kesi ya Semenya

Semenya, ambaye anaainishwa kama mtu mwenye utofauti katika ukuaji wa jinsia, lakini ambaye ametambuliwa wakati wote kama mwanamke kisheria, amekataa kutumia dawa za kupunguza viwango vyake vya testosteroni, tangu Shirikisho la Riadha lilipoanzisha sheria hizo mwaka 2018