1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seneta Jeanine Anez ajitangaza kuwa kaimu rais, Bolivia.

Tatu Karema
13 Novemba 2019

Naibu spika wa baraza la seneti nchini Bolivia Jeanine Anez amejitangaza kuwa kaimu rais wa nchi hiyo, kufuatia hatua ya rais Evo Morales kujizulu na kuikimbia nchi.

https://p.dw.com/p/3Suox
Bolivien, La Paz: Boliviens Senatorin Jeanine Anez
Picha: picture-alliance/dpa/J. Karita

Raia wa Bolivia sasa wanakabiliwa na  hali isiyoeleweka baada ya seneta kutoka kambi ya upinzani Jeanine Anez kujitangaza kuwa kaimu rais wa taifa hilo linalokumbwa na mzozo saa chache baada ya aliyekuwa rais Evo Morales kuikimbia nchi na kutafuta hifadhi nchini Mexico. Yapo maswali ambayo bado hayana majibu kuhusu nani atakayeshirikiana na Anez wakati wafuasi wa Morales wakimshtumu kwa hasira kwa kujaribu kuchukuwa mamlaka kutokana na tangazo lake la jana na kuzua uwezekano wa matatizo zaidi kufuatia wiki za mivutano kuhusiana na uchaguzi mkuu wa urais wa tarehe 20 mwezi Oktoba.

Makundi ya watu yalimiminika barabarani wakishangilia na kupeperusha bendera za taifa hilo jana usiku baada ya Anez kuchukuwa wadhifa wa kiongozi wa bunge la seneti, wadhifa unaofuatia ule wa urais. Wafuasi wa Morales waliokuwa na ghadhabu walijibu kwa kulazimisha kuingia katika jengo la bunge mjini La paz wakipiga kelele za kumtaka Anez aondoke.

Anez, mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na aliyekuwa mtangazaji katika runinga alionekana kuwa katika nafasi hafifu. Alijitangaza kuwa kaimu rais ijapokuwa hakukuwa na idadi ya wabunge wanaohitajika katika bunge la seneti baada ya wabunge wa chama cha Morales kukosa kuhudhuria kikao hicho. Hakuapishwa na mtu kabla ya kujitokeza katika ukumbi wa ikulu ya zamani ya rais akiwa amevalia ukanda wa urais na kusema

Wakati huo huo, Marekani imesifu kuondoka kwa aliyekuwa rais Evo Morales ikisema ni hatua nzuri. Hii ni kulingana na afisa mmoja mkuu katika serikali ya Rais Donald Trump aliyesema haya  Jumanne. Afisa huyo alisema kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kutuliza hali ilivyo nchini Bolivia na kuongeza kwamba Mexico iliiarifu Marekani kuhusu nia yake ya kumpa Morales Hifadhi na Marekani ikatoa usaidizi wake katika kufanikisha hatua hiyo.

Huku hayo yakijiri, taarifa kutoka wizara ya ndani ya Marekani imetoa agizo kwa jamaa za wafanyikazi wa Marekani nchini Bolivia kuondoka nchini humo kutokana na ghasia hizo zinazoendelea  katika taifa hilo la Amerika ya Kusini. Wizara hiyo pia imeonya raia wa Marekani dhidi ya kusafiri kuelekea Bolivia na kusema kuwa Marekani haina uwezo wa kutosha kutoa huduma za dharura baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata kusababisha maandamano yaliosababisha kujiuzulu kwa Evo Morales kama rais wa nchi hiyo siku ya Jumapili.