1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serbia kwenda mahakama ya The Hague

11 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CaIl

BELGRADE.Serbia imesema kuwa itapinga hatua ya kutaka kujitenga kwa jimbo lake la Kosovo linalotaka kujitangazia uhuru.

Rais Boris Tadic wa Serbia amesema kuwa iwapo hilo litatokea watalifikisha katika mahakama ya kimataifa ya sheria ya mjini The Hague.

Urusi kwa upande wake ambayo inaiunga mkono Serbia imesema italitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutengua maamuzi yoyote ya upande mmoja juu ya uhuru wa Kosovo.

Matamshi hayo yamekuja huku muda wa mwisho uliyowekwa na Umoja wa Mataifa kwa pande mbili zinazozozana juu ya uhuru wa Kosovo kufikia muafaka ukikaribia kumalizika.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wameonya kuwa uhuru kwa jimbo la Kosovo ni jambo la hatari litakalopelekea kunazishwa kwa vikundi vingi vya wanaharakati katika eneo lote la Ulaya.