1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali mpya ya Ivory Coast itatangazwa leo hii

23 Februari 2010

Waziri Mkuu Guillaume Soro, hii leo anatazamiwa kuitangaza serikali mpya ya Ivory Coast. Inatumainiwa kuwa hatua hiyo itasaidia kumaliza maandamano ya machafuko yaliyoenea sehemu mbali mbali nchini humo.

https://p.dw.com/p/M90V
Guillaume Soro, new prime minister of Cote d'Ivoire, speaks at the prime minister's office in Abidjan on April 4, 2007. Soro came into office on Wednesday. He was officially designated as prime minister by President Laurent Gbagbo on March 29. Foto: Xinhua +++(c) dpa - Report+++
Waziri Mkuu wa Ivory Coast, Guillaume Soro.Picha: DPA
Rais wa Burkina Faso Blaise Compaore amefanikiwa kuwapatanisha mahasimu wakuu ili kumaliza mzozo wa kisiasa nchini Ivory Coast. Baada ya kuwa na majadiliano marefu katika mji mkuu wa Ivory Coast Abidjan, mpatanishi Compaore alisema mahasimu wakuu wawili wamekubali kuunda serikali mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ili kuweza kupanga tarehe ya kufanywa uchaguzi wa rais
Ivory Coast President Laurent Gbagbo gestures during a news conference in Paris, Sunday Jan. 26, 2003. Gbagbo called for a restoration of order and calm at home, asking Ivorians to restrain from demonstrations that erupted in the West African nation's capital Abidjan over a French-brokered peace accord to end a four-month civil war. (AP Photo/Francois Mori)
Rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo.Picha: AP
Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo aliivunja serikali ya Waziri Mkuu Guillaume Soro na Tume ya Uchaguzi hapo Februari 12 na hivyo kusababisha machafuko katika nchi iliyogawika kati ya kusini na kaskazini. Machafuko hayo yalizusha wasiwasi mpya iwapo nchi hiyo ya Afrika Magharibi itaweza kuwa na uchaguzi wa rais katika mwezi wa Machi kama ilivyopangwa. Uchaguzi huo umeshaahirishwa mara sita tangu muhula wa Rais Gbagbo kumalizika katika mwaka 2005. Waziri Mkuu Soro alipozungumza na waandishi wa habari mjini Abdjan alisema baraza jipya la mawaziri wake litatangazwa leo hii na baadae watakuwa na mkutano. Amesema, majadiliano ya upatanishi yamemalizika na yametoa fursa kwa viongozi kumaliza mzozo wao na kuendeleza mchakato wa kurejesha amani nchini humo. Lakini Alphonse Djedje Mady wa kundi kuu la upinzani RHDP akieleza wasiwasi wake kuhusu makubaliano hayo na jinsi yatakavyotekelezwa, amesema kuwa majadiliano yangali yakiendelea. Suala kuu linahusika na muundo wa Tume Huru ya Uchaguzi. Upinzani unasema, Tume ya Uchaguzi iundwe kabla ya serikali mpya. Hivi karibuni pia wapinzani wametoa mwito wa kumtaka Gbagbo ajiuzulu. Waziri Mkuu Soro aliejaribu kuunda serikali mpya alikumbana na upinzani mkali kutoka kwa viongozi mashuhuri wa upinzani, Henri Konan Bedie na Alassane Quattar waliokuwa rais na waziri mkuu wa zamani wa Ivory Coast. Viongozi hao walishindwa kuafikiana walipokutana siku ya Jumapili katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou. Lakini siku ya Jumatatu, Rais wa Burkina Faso katika jitahada ya kuleta maafikiano alikwenda Ivory Coast na alifanikiwa kuleta maafikiano kati ya makundi hasimu. Gbagbo aliivunja serikali ya Soro ya umoja wa taifa na Tume ya Uchaguzi akiituhumu tume hiyo kusajili majina ya uongo huku upinzani ukimtuhumu rais kuwa anajaribu kuchelewesha uchaguzi. Hasira ya umma inazidi kila uchaguzi unapoahirishwa. Lengo la uchagauzi huo ni kuleta umoja katika taifa lililogawika kati ya kusini linalodhibitiwa na chama cha Gbagbo na upande wa kaskazini unaodhibitiwa na chama cha zamani cha waasi New Forces Party cha Soro tangu jaribio la kutaka kumpindua Gbagbo katika mwaka 2002 kutofanikiwa. Mwandishi: P.Martin/AFPE/RTRE Mhariri: Abdul-Rahman, Mohammed