1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya kupinga uamuzi wa mahakama kuzuia polisi kwenda Haiti

26 Januari 2024

Serikali ya Kenya imesema itapinga uamuzi wa mahakama ulioizuia kupeleka maafisa wa polisi nchini Haiti kuongoza kikosi kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kulisaidia taifa hilo kukabiliana na vurugu za magenge.

https://p.dw.com/p/4bjDJ
Mahakama ya Juu ya Kenya.
Mahakama ya Juu ya Kenya.Picha: Yasuyoshi Chiba/AFP

Msemaji wa serikali, Isaac Mwaura, ameeleza katika taarifa yake kuwa serikali inaheshimu utawala wa kisheria na hivyo wamepanga kuwasilisha rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama.

Mapema leo, Mahakama Kuu ilitoa uamuzi wa kuizuia serikali kupeleka maafisa wa polisi nje ya nchi na kuitaja hatua hiyo kuwa kinyume na katiba.

Soma zaidi: Mahakama Kenya yaizuwia serikali kupeleka askari Haiti

Jaji wa Mahakama Kuu, Chacha Mwita, amesema katika uamuzi wake leo kuwa jeshi la ulinzi la Kenya (KDF) ndilo pekee lenye uwezo wa kuongoza ujumbe wa amani nje ya nchi.