1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEVILLE: Russia yapinga hatua ya Marekani kuweka mitambo ya ulinzi, Ulaya Mashariki.

10 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTT

Waziri wa Ulinzi wa Russia, Sergei Ivanov, amesema hakuna haja ya Marekani kuweka mitambo ya ulinzi ya kukinga makombora katika eneo la mashariki mwa Ulaya.

Waziri huyo alikuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Seville, Uhispania baada ya mkutano wa mawaziri wa Ulinzi wa Umoja wa Ulaya.

Sergei Ivanov alisema Poland na Jamhuri ya Czech hazimo katika eneo zuri la Marekani kujikinga na shambulio kutoka Korea Kaskazini au Iran.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Robert Gates, amesema haoni sababu za Russia kupinga mpango huo wa ulinzi wa Marekani.

Waziri Sergei Ivanov alisema Russia itarekebisha mifumo yake ya ulinzi kuhakikisha kwamba itaendelea kutenda kazi ipasavyo.