1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio la risasi lachochea maandamano Hong Kong

Admin.WagnerD2 Oktoba 2019

Maandamano makubwa yametokea mjini Hong Kong wakati hasira zikizidi kupanda miongoni mwa waandamanaji kufuatia tukio la polisi kumpiga risasi mmoja ya muandamanaji kijana anayesemakana alimshambulia afisa huyo.

https://p.dw.com/p/3QdKa
Hongkong Proteste
Sehemu ya waandamanaji mjini Hong KongPicha: picture-alliance/AP Photo/K. Cheung

Kisa hiki kimeongeza ghasia zinazoukumba mji huo kwa miezi kadhaa. Amina Abubakar na taarifa zaidi.

Maelfu ya waandamanaji wakiwemo wafanyakazi wa maofisini waliovali suti na mashati, walikusanyika katika uwanja mmoja kabla ya kuanza kuandamana mjini humo huku wakitoa maneno ya kuikashifu serikali pamoja na polisi.

Saa chache kabla ya maandamano hayo makubwa, mamia ya wanafunzi walikusanyika katika shule ya kijana wa miaka 18 Tsang Chi-kin, aliyepigwa risasi kifuani  na polisi wakati yeye na wanafunzi wengine waliovalia vitambaa vya kufunika uso walipowashambulia maafisa wa polisi kwa kutumia myanvuli na magongo.

Vidio ya tukio hilo ilisambaa kwa kasi mno katika mitandao ya kijamii na kuzua ghadhabu kubwa miongoni mwa waandamanaji.

Raia wa Hong Kong wasema "Tumechoka"

Hongkong Proteste in Tsuen Wan
Picha: AFP/P. Wong

Hong Kong eneo la kimataifa la kibiashara lipo katika taharuki kufuatia tukio hilo, ambapo ni mara ya kwanza kwa muandamanaji kupigwa risasi katika maandamanmo  ya kudai demokrasia zaidi yanayoendelea kwa takriban miezi minne.

"Watu wa Hong Kong wamechoshwa na maneno ya kulaumiwa wakati wakijaribu kujikinga na risasi za moto na bunduki," alisema muandamanaji mmoja aliyefunika uso wake wakati wa mkutano na waandishi habari karibu na shule ya Tsang.

Hong Kong iliendelea kupitia mgogoro mkubwa wa kisiasa hapo jana wakati China iliposheherekea miaka 70 ya utawala wa chama cha kikomunisti  kukiwa na gwaride kubwa la kijeshi mjini Beijing.

Makumi ya watu wapandishwa kizimbani

Carrie Lam in HongKong
Kiongozi wa Hong Kong, Carrie LamPicha: picture-alliance/AP Photo/K. Cheung

Hii leo waandamanaji 96 waliokamatwa wakati wa vurugu zilizotokea siku ya Jumapili wamefikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa makossa ya kusababisha Ghasia hii ikiwa ni kulingana na stakabadhi za  mahakamani.

Miaka ya walioshitakiwa ni kati ya miaka 14 hadi 39.

Maandamano hayo yalianza kufuatia mpango ambao sasa umefutiliwa mbali wa kuwapelewa wahalifu kushitakiwa China bara, lakini baada ya viongozi kutochukua hatua maandamano yaligeuka na kuwa maandamano makubwa ya kudai demiokrasia zaidi.

Huku hali ikizidi kuwa tete mjini Hong Kong kiongozi wa Mji huo Carrie Lam, anaonekana kutotaka kupata suluhusu ya mgogoro wa kisiasa huku polisi wakizidi kupambana na waandamanaji sugu.

Kati ya Matakwa yao ni uchunguzi huru juu ya hatua za polisi na msamaha kwa wale waliokamatwa mambo ambayo  Lam amesema hawezi kuyakubali.