1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ILO yaonya ongezeko la watu wanaofanya kazi za kulazimishwa

19 Machi 2024

Shirika la Kazi la Duniani (ILO) limeonya kuhusu ongezeko la idadi ya watu wanaofanya kazi za kulazimishwa pamoja na faida kubwa itakonayo na vitendo hivyo vya unyonyaji.

https://p.dw.com/p/4duKs
Pakistan
Mtoto wa Pakistan akifanya kazi katika duka la chaiPicha: Mohammad Sajjad/AP Photo/picture alliance

Shirika la Kazi la Duniani (ILO) limeonya kuhusu ongezeko la idadi ya watu wanaofanya kazi za kulazimishwa pamoja na faida kubwa itakonayo na  vitendo hivyo vya unyonyaji. Shirika la ILO limesema kazi ya kulazimishwa katika sekta binafsi, huzalisha dola bilioni 236 za faida haramu kila mwaka.

Soma: ILO: Wanawake bado wataabika kupata ajira

Tangu mwaka 2014, jumla ya faida hizo haramu ziliongezeka na kufikia dola bilioni 64, hii ikiwa ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaolazimishwa kufanya kazi lakini pia faida kubwa inayopatikana kutokana na vitendo hivyo.

Ukahaba wa kulazimishwa ulichangia faida hizo kwa asilimia 73. Kazi ya kulazimishwa na faida haramu huzingatiwa pale tu mtu hulipwa kiwango hafifu kuliko kile alichostahili iwapo angejumuishwa kwenye mfumo rasmi wa kazi. Mataifa ya Asia ya Kati na Ulaya yametajwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu wanaofanya kazi za kulazimishwa.