1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirika la utangazaji nchini Zimbabwe mikononi mwa jeshi

Zainab Aziz
15 Novemba 2017

Wanajeshi nchini Zimbabwe wamelitwaa shirika la utangazaji la serikali ZBC katika mji mkuu Harare na hivyo kuongeza kuenea kwa uvumi wa kuangushwa serikali ya rais Robert Mugabe. Hata hivyo jeshi limekanusha uvumi huo.

https://p.dw.com/p/2ne9X
Zimbabwe Soldaten vor Harare
Picha: Reuters/P. Bulawayo

Wiki iliyopita rais Mugabe alimfukuza kazi makamu wake Emmarson Mnangagwa. Mkuu wa majeshi ya Zimbambwe jenerali Constatino Chiwenga aliijibu hatua ya kufukuzwa makamu wa rais bwana Mnangagwa kwa kutishia kukomesha kampeni ya kuwafukuza wanachama wa chama kinachotawala cha ZANU PF na alisema jeshi liataingilia kati iwapo italazimika. Jenerali Chiwenga amesema lazima wale wanaoendesha kampeni ya usaliti wakumbushwe kwamba inapobidi kuyalinda mapinduzi ya watu wa Zimbabwe jeshi halitasita kuingilia kati. Hata hivyo chama cha ZANU PF kimejibu kauli ya Jenerali Chiwenga kwa kuiita kuwa ni uhaini na kueleza kwamba hakitasalimu amri mbele ya vitisho.