1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shughuli za Hijja za mwaka huu za anza

Siraj Kalyango17 Desemba 2007

Mahujaji zaidi ya 2 millioni ndio wanakisiwa kushiriki

https://p.dw.com/p/CcqN
Mamia kwa maelfu ya mahujaji wa Kiislamu wakizunguka Kaaba ilio ndani ya msikiti wa Makka -Saudu ArabiaPicha: AP

Waumini wa dini ya kiislamu wapatao millioni mbili wameanza rasmi shughuli za Hijja za mwaka huu jumatatu.

Ulinzi mkali umeimarishwa pamoja na utaratibu mpya ili kuepuka visa vya ghasia kama vya mwaka jana ambapo watu wasiopungua 300 waliuliwa katika mkanyagano katika maeneo takatifu.

Mwanzo wa shughuli unatokea wakati mahujaji wanapoanza safari maalum kutoka mji wa Mecca,nchini Saudi Arabia, na kuelekea katika bonde la Mina, umbali wa kilomita tano -mashariki mwa mji mtakatifu kwa waislamu wa Mecca.Mahujaji hao, wake kwa waume, wakiwa wamevalia shuka nyeupe,wameanza safari muhimu ya kufuata nyayo za Nabii Muhammad, miaka zaidi ya 1,400 iliopita.

Wengi wa mahujaji wameondoka Mecca kwa kutumia usafiri mbalimbali mkiwemo, magari pamoja na kutembea kwa mguu.Wanatarajiwa kumaliza usiku mmoja wa kuamkia kesho katika eneo la Mina.Hata hivyo sio lazima wote kukaa hapo.Wengine watafululiza hadi mlima wa Arafat.

Shirika la habari la Saudi Arabia, SPA-linasema kuwa usalama umeimarishwa na pia kuweka waongozaji wa kutosha katika maeneo hayo ambayo kawaida huzusha maafa.Pia mgari ya wagonjwa na watoaji wa huduma ya kwanza.Utawala wa Saudia umajaribu mara hii kuweka vitendea kazi tosha kwa mahujaji kama vile kupanua njia wanakopitia wakifanya miiko ya kidini.Mwaka wa 1990 mahujaji zaidi ya elf moja walipoteza maisha yao katika mkanyagano uliosababishwa na waumini kutaka kutekeleza miiko fulani.

Mwaka jana pia katika eneo la Mina watu 364 walifariki pia baada ya mkaganyagano uliotokea katika mlango wa daraja la Jamarat ambako kunafanyika shughulia ya kutupa mawe kama ishara ya kumpiga shetani.

Mara hii kumefanyikwa marekebisho ambapo kumwekwa sehemu nyingine katika daraja hilo kwa lengo la kurahisisha mahujaji.

Wakuu wa Saudia wanasema kuwa sasa kijidraja hicho kinaweza watu zaidia ya laki mbili kwa saa.Idadi kamili ya mahujaji wa mwaka huu,haijaulikani,lakini shrika la habari la SPA limesema kuwa watu wanaofikia millioni 2 ndio wametoka nje kwenda kuhiji. Kati ya hao ni rais wa Iran Mahmood Ahmed- nejad ambae anasubiriwa kuhiji mwaka huu.

Rais Nejad anasemekana amealikwa na mfalme Abdullah wa Saudi Arabia.Hi ndio itakuwa mara ya kwanza kwa rais wa jamhuri ya kiislamu wa Iran kuhiji akiwa ofisini.

Kuhiji kwake kunaonekana kama muhimu uhusiano kati ya tawala mbili haukuwa mzuri.Watawala wa nchi hizo mbili wote ni waislamu lakini wa madheebu tofauti.Watawala wa Iran ni wa Shia ilhali wa Saudi Arabia ni wa Sunni.

Julai mwaka wa 1987, kulifanyika maandamano ya wa Iran wakatiwa hijja na tukio hilo lilisababisha nchi hizo mbili kuvunja uhusiano wa kidiplomasia.Vikosi vya usalama vilipojaribu kuvunja maandamano hayo, na katika purukushani iliofuata,watu 402 walikufa wakiwemo wairan 275.Tangu wakati huo mahujaji wa Iran walisusia hija hadi mwaka wa 1991.

Shughuli rasmi za hijja zinamalizika Ijumaa ya wiki hii.Hijja ni sehemu ya nguzo tano za dini ya kiislamu na ni wajibu wa kila muislamu angalau kuhiji mara moja maishani mwake ikiwa anauwezo.